Matthew 7

1Usihukumu, nawe usije ukahukumiwa. 2Kwa hukumu unayohukumu, nawe utahukumiwa. Na kwa kipimo unachopima na wewe pia utapimiwa hicho hicho.

3Na kwa nini unatazama kipande cha mti kilichoko kwenye jicho la ndugu yako, lakini hutambuwi kipande cha gogo ambalo limo katika jicho lako? 4Unawezaje kusema kwa ndugu yako, ngoja nikutolee kipande kilichomo kwenye jicho lako, wakati kipande cha gogo kimo ndani ya jicho lako? 5Mnafiki wewe; kwanza toa gogo lililomo kwenye jicho lako, na ndipo utakapoweza kuona vizuri na kukitoa kipande cha mti kilichomo kwenye jicho la ndugu yako.

6Usiwape mbwa kilicho kitakatifu, na usiwarushie nguruwe lulu mbele yao. Vinginevyo wataviharibu na kuvikanyaga kwa miguu, na tena watakugeukia wewe na kukurarua vipande vipande.

7Omba, nawe utapewa. Tafuta, nawe utapata. Bisha hodi, na wewe utafunguliwa. 8Kwa yeyote anayeomba, hupokea. Na kwa yeyote anayetafuta, hupata. Na kwa mtu ambaye anayebisha hodi, atafunguliwa. 9Au kuna mtu miongoni mwenu ambaye, ikiwa mtoto wake amemwomba kipande cha mkate atampa jiwe? 10Au ikiwa atamwomba samaki, na yeye atampa nyoka?

11Kwa hiyo, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, Je! Ni kiasi gani zaidi Baba aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wanao muomba yeye? 12Kwa sababu hiyo, unapotaka kufanyiwa kitu chochote na watu wengine, nawe pia itakupasa kuwafanyia hivyo hivyo wao. Kwa kuwa hiyo ni sheria na manabii.

13Ingieni kwa kupitia geti jembamba. Kwa kuwa geti ni pana na njia ni pana inayoongoza kwenye uharibifu, na kuna watu wengi wanaopitia njia hiyo. 14Geti ni jembamba, Geti jembamba ni njia inayongooza katika uzima na ni wachache wanaoweza kuiona.

15Jihadhari na manabii wa uongo, wanaokuja wamevaa ngozi ya kondoo, lakini kweli ni mbweha wakali. 16Kwa matunda yao mtawatambua. Je watu wanaweza kuvuna matunda kwenye miba, au mtini kwenye mbengu ya mbaruti? 17Kwa jinsi hiyo, kila mti mzuri huzaa matunda mazuri, lakini mti mbaya huzaa matunda mabaya.

18Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. 19Kila mti ambao hauzai matunda mazuri utakatwa na kutupwa katika moto. 20Hivyo basi, utawatambua kutokana na matunda yao.

21Si kila mtu aniambiaye mimi, ‘Bwana, Bwana,’ ataingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yule pekee atendaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22Watu wengi wataniambia siku hiyo, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako, hatukutoa mapepo kwa jina lako, na kwa jina lako tulifanya matendo mengi makuu?’ 23Ndipo nitawaambia wazi, ‘sikuwatambua ninyi! Ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu!’

24Kwa hiyo, kila mmoja asikiaye maneno yangu na kutii atafanana na mtu mwenye hekima aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. 25Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, na upepo ukaja na ukaipiga nyumba hiyo, lakini haikuweza kuanguka chini, kwa kuwa ilikuwa imejengwa juu ya mwamba.

26Lakini kila mtu anayesikia neno langu na asilitii, atafananishwa na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga. 27Mvua ikaja, mafuriko yakaja, na upepo ukaja na kuipiga nyumba hiyo. Na ikaanguka, na uharibifu wake ukakamilika.”

28Ulifika wakati ambao Yesu alipomaliza kuongea maneno haya, makutano walishangazwa na mafundisho yake, kwa kuwa alifundisha kama mtu mwenye mamlaka, na si kama waandishi wao.

29

Copyright information for SwaULB